Skip to main content

Featured

Liagaana kuloohiza miyiinzi jia Lulogooli

Liagaana 1 (12/01/2024) Avaali hao 1. Lung'afa Igunza 2. Pam Igara 3. Rhoda Obwoyere 4. Mw. Obwoyere 5. Alfred Ogola 6. Pharrex Comfort 7. Bernard Ngoda 8. Kelonye Festus Liloohiza Avaagaani vavugiilizani kuzyizagilila na miyiinzi jia kuzuva Ululogooli muvandu Vamanyi kandi vavoola kuvezaa na ligaana haimbi ku haimbi (onlaini), kutaanga na vuli lisiiza Vamanyi vavitiza ni vulahi kuve na ikamati ia vusololi/miandu kigila imiyiinzi gaenyaa jikolwe

Kuli liita "Maragoli" liataanga [Jinsi jina "Maragoli" lilivyoanza]


Hakilivwa, esukuulu ea vusiza, South Maragoli.

Ehiiri eosieosi mukivala enyoolaa liita kuvitila zinzila vili; nigatali vandu vaene valinyoole kutulana na kuli vaene vailaangaa, kuduuka live litulanaa na zihiiri ziteende. Kunyi iliita “Maragoli”, ni girigari liatulana na vateende kuli vaakulaanga. Kanyiingi iliita ilio limanya livula kuva na kivuni muehiili elaange. Valala vamanya vazyizagirira kulivugiirira iliita ilio (kuli “Bushman” kutula South Africa) na avandi kulisuula (kuli “Kistosh” lia Bukusu).

Jamii yoyote duniani hupata jina lake kupitia njia mbili, kama sivyo wanajamii wapate jina hili kwa namna wanaovyojiita wenyewe, basi itakuwa inachangiwa na jamii jirani wanavyowaita. Na kwetu sisi jina la “Maragoli”, bila shaka ni majirani walivyotuita. Wakati mwingi jina hilo huwa na maana isiyotambulika vizuri na wenyeji. Wengine waweza kuendelea kulikubali jina hilo (k. m. “Bushman” Afrika Kusini) na wengine kulikataa (k. m. “Kitosh” Wabukusu).

Vutaangiru vua liita “Maragoli” silimanyikani vulahi, nitali kunyala kutunyiiriza kuli linyala kuva liatulila. Kuluvega lua kivuni, noho ilimanyika kukunyi, ling'ana “Maragoli” ni lilala na liita lia vandu Valogooli na kandi havamenyi Evulogooli. Galolekaanga iliita “Maragoli” livugulaanga gaosi gaviri; havuundu na vandu.

Asili ya jina “Maragoli” haijulikani vyema ingawa tunaweza kukisia jinsi jina hilo lilivyotokea. Kwa upande wa maana, au kwa ufahamu wake miongoni mwetu, jina “Maragoli” ni sawia na majina ya jamii kama Walogooli (wanajamii) na Evulogooli (sehemu wanakoishi). Inamaanisha kuwa jina “Maragoli” huchukua yote mawili; sehemu na watu.

Kuluvega lua liloombeka, galaloleka iliita “Maragoli” liveeye na zingedu ziviri; “ma-” na “-ragoli”. Muesayaanzi ea lulimi, kuvoolaanga izingedu ziloombaa ling'ana ni “emofiimu” (vunyiingi ziva “zimofiimu”). Ku ndyo iling'ana “Maragoli” livee na zimofiimu ziviri: umutwi gwa ling'ana “ma-” na umuviri gua lio, “-ragoli”.

Kwa upande wa maumbo nao, pia ni jambo la dhahiri kuwa neno la “Maragoli” linapatikana kuwa na sehemu mbili: “ma” na “ragoli”. Katika sayansi ya lugha yaani isimu, tunasema kwamba hivi vipashio vidogo vidogo katika neno moja vinaitwa mofimu (umoja wake pia unaitwa mofimu). Kwahiyo neno la “Maragoli” lina mofimu mbili: kiambishi-awali cha “ma-” na shina la nomino “-ragoli”.

Leka kutaange na “‑ragoli”. Lilola lia “ragoli” lilolekaanga vulahi kutulana na zihiiri zivoolekaa ziasaanga uvuiko na Mulogooli. Ehiiri evoolekaanga kuva haimbi muno na Valogooli ni ea Vakisyi (Gusii). Na Mulukisyi vatalaanga “Omoragori” kuli umwiimiriri ua lisuuvila, umulogi mulilola lindi (Getuma 2016:25).  Egaasi ea Omoragoli ni kutala vilolekizu na kandi kugaanga. Aga gazyaanaa na limanyikana lia Mulogooli, avoolekaanga yaali umundu ua lisuuvila linene.

Hebu tuanzie na “‑ragoli”. Dhana hii ya “ragoli” itajulikana vyema tukiangalia jamii ambayo Mulogooli alifuatana nao. Jamii ambayo inasemekana kuwa karibu zaidi na Maragoli ni ya Kisii. Na katika lugha ya Kikisii, watu wanataja “Omoragori” kama kiongozi wa imani (Getuma 2016:25) - kwa lugha ya Kiswahili Sanifu basi mlozi ukipenda. Kazi ya “Omoragori” ni kufuta bao yaani kupiga ramli na hata kufanya uganga. Sifa hizo zinaendana na zile za Mulogooli ambaye pia anayesemekana kuwa mtu wa imani ya kidini.

Ulu kugelize kumulika hake ikitivuku kia “ma-”, na limanya ndi ganyalikaa kuva ilitulana lia kio ni vinyiingi kinga kutulana na Lulogooli, Luswahili noho Luvo (Lujaluo).

Sasa tujaribu kukimulika kidogo kipashio cha “ma-”, ila tujue kwanza kuwa inawekezekana vyanzo vya kiambishi hiki labda ni vingi haswa kutoka Kimaragoli chenyewe au kutoka Kiswahili au kutoka Kijaluo.

Mululogooli, kitivuku kia “ma-” kiveeye na vivuni viviri vinene. Kivuni kia kutaanga kilolekelaanga mulihuumbi lia vilaange lia sita [sw.: ngeli ya 6 {ma}]. Lihuumbi ilio ni lia vilaange muvunyiingi. Amang'ana gaa vilaange zana gaveeye kuli masaanda, mavuyu na gandi. Kivuni kinene kia kaviri ni ilitala kindu kilogooli muvunyiingi; kuli kiukulya na emu. Ulalola kuvoola maduuma malogooli, mabwooni malogooli na gandi. Yili liveeye na kivuni kia vutaangilu vua kindu ikio.

Katika Lulogooli, lugha Kimarogoli yenyewe inavyotajwa, kiambishi cha “ma-” kina maana mbili kuu. Maana ya kwanza inajitokeza kwenye ngeli ya 6 {ma}. Ngeli hiyo haswa ni ya nomino kwa wingi. Mfano ni lisaandamasaanda (kucha-makucha), livuyu - mavuyu (yai – mayai) na kadhalika. Maana kuu ya pili ni kwa nomino inayoelezea kitu cha zama, kama mbegu au chakula, litapata jina lilogooli (mbegu ya kimaragoli) na malogooli (uwingi wa mbegu ya kimaragoli). Hii ikiwa na maana ya asili ya kitu hicho.

Kuluvega lua litulana na Luvo, histuri muvuimbi ni kuva ehiiri ea Valogooli eakolaanga kugulizanilana vindu na Vavo mukitu Kisumu, kikikili kia kuala vuzwa. Kali lulala gavooleka iliita lia kitu zana liatulana na liita lia Lulogooli, kusuma, liveeye na kivuni kia “kunyoola iviukulya echoova ewa engo na kuilana na vio”. Avagulizi kutula Evulogooli kuduuka vave vaatalaa amaita gaviavaagulizaa. Kuli; maduuma malogooli, mabwooni malogooli na vindi. Ganyalikaa vaaduuka havundu valaangwa “Malogooli” na vagulizi vache.

Kwa upande wa ushawishi wa Kijaluo, historia kwa ufupi ni kwamba jamii ya Maragoli ilikuwa inafanya biashara na jamii ya Luo kwenye soko kuu la Kisumu, hata kabla ya mji wa Kisumu wa kisasa kuwepo. Inakisiwa kwamba jina la soko hili lilitokana na neno kusuma la lugha ya Kimaragoli ambalo linamaanisha “kupata vyakula na kurudi navyo nyumbani”. Wanabiashara watokao Maragoli huenda wakatangaza sana bidhaa zao kwa mkazo wa asili yao ya Maragoli, kama maduuma malogooli (mahindi ya Kilogooli), mabwooni malogooli (viazi vitamu vya Kilogooli) na kadhalika. Inawezekana matumizi haya mengi ya Malogooli yalipelekea hata wafanyabiashara hao wakaitwa “Malogooli” na wenzao sokoni.

Avagulizanili Vavo avao, vaveeye ehiiri eteende, vaanalilaa kulaanga vandu vaa Bantu kuli Markakamega (vaa kutula Kakamega), Marabandu (vaa kiluhya, “Abantu”) na gandi. Ikitivuku kia kivoho “Mar-” kikola kutumika kuli “vandu na luvega lua vatulaa”. Muliloohiza ili, niuunga kikolwa ‑logola noho ‑lagula ulanyoola Marlogola na Marlagula. Na lua limoloma likolaa kunyagula, embya eindi emanya etulila, etageeheraa liita, Maragoli.

Hao wafanyabiashara Wajaluo, wakiwa jamii jirani, walijulikana kuita watu wa jamii mbalimbali za Wabantu kwa majina ya “mar fulani fulani”. Hata siku ya leo kwa maneno ya Markakamega (wa kutoka Kakamega), Marabandu (wa kutoka sehemu za Uluyani) na kadhalika. Kwa muundo huu, mkiunganisha kitenzi-mizizi cha kuroga yaani -logola (au -lagula kwa sababu ya tofauti baina ya lahaja za viluyia) mtapata “Marlogola” (au “Marlagula”). Hivyo, haingekuwa ajabu sana neno likabadili kuwa Maragoli kwa sababu ya matamshi tofauti tofauti enzi za zamani.

Sikuali mukiitu mueng'ine ewa Vavo na Valogooli vaagaaniliraa. Kali muvuiko, vamanyikana hanene kuli valamwa [Sw.: mashemeji]. Na sivaadaka ku linyaangizana, kigila gavoolekaanga luvega kuli Chulaimbo luali na kivuni, “Ilana Embo!”, luene lua Valogooli vaakubana na vao. Na kigila Avavo valaangaanga uvulwaani “gore”, kuduuka vave vaalaanga avalogooli “Margore” - avakubani.

Na si kwa biashara tu ambapo Waluo na Wamaragoli walipatana. Pia kwenye ukoo, wakajulikana sana kuitana “mashemeji” hadi hii leo. Lakini si sahihi kwamba hawajawahi kuwa na mvutano, inasemekana jina la kijiji cha Chulaimbo lina maana ya “Rudi Uluoni!”, pale Wamaragoli walipigana nao. Tukifuata mantiki hii, pia tukumbukwe hata Wajaluo huita vita “gore”, basi haukosekani uwezekano wa Wamaragoli waliotajwa “Margore” katika historia, kumaanisha wanavita.

Muluswahili, ilitumika lia kitivuku “ma-” ni kuvugiza havundu. Ling'ana kuli “Makwao” liveeye na kivuni kia havundu haa vao. Ling'ana lindi kuli “Madachi” litulanaa na avandu kutula kivala kia Dutch, avangeresa. Ndyo kandi iling'ana “Maragoli” lilamanyya vandu na havuundu. Ku uluo niiva Luswahili luasaanga muyaga, indio gaaiza. Ululimi lua Valogooli luamanyikana kuli “Ragoli” eng'inga ea ling'ooda na Friends Africa Mission, 1907. Na amang'oda gaa Luswahili gaali gaa vukonyi hanene mulikoonya kumanya ilimoloma lia zihiiri zindi zia Bantu.

Kwa Kiswahili, moja ya matumizi ya ma- ni kujulisha pahali. Neno kama “makwao” au “makaazi”, tukiacha umbo la “-kwao” au “-kaazi” tubaki na umbo la “ma-” tujue hakika hii inamaanisha pahali. Neno lingine kama “madachi” linatokana na “ma-” na “-dachi” na hapo “ma-” inamaanisha uwingi wa watu na “-dachi” kumaanisha The Dutch kwa Kiingereza ila wakati huo zamani “madachi” pia lilimaanisha Wajerumani. Neno “Maragoli” basi lina maana ya sehemu, watu au zote kwa pamoja vivyo hivyo linavyotumika hivi sasa. Na ikiwa Kiswahili kilichangia pakubwa, basi chaweza kuwa sababu kuu ya kiambishi “ma-” cha pahali. Pamoja na kuwa lugha ya Kimaragoli ilijulikana kama “Ragoli” wakati wa uandishi wa kwanza na Friends Africa Mission, 1907 kutolewa. Hii “ragoli” iliwezekana kuwekwa “ma” kwa sarufi ya Kiswahili kwa sababu Kiswahili ilitumika pakubwa kwa marejeo ya maandishi ya lugha za Kibantu.

Hake vuzwa lua amang'ooda gaa “Luragoli” gaali gatulaa, ling'ana “Maragoli” liamanya lihile miri. Lola kuli P.O. BOX 50300 Maragoli. Lola kandi vigulu via Mungoma viamanya vilaangwe Maragoli Hills. Kali ehiiri ea Valuhya muvunene eamanya emanyikane na vandi kuli (kuli Avakuria) vuzwa Maragoli. 

Punde tu baada ya maandishi yaliyoamuliwa, basi haukupita muda mrefu pale jina la Maragoli likashika mizizi sana. Mfano ni sanduku la posta P.O. BOX 50300 Maragoli. Mfano mwingine ni milima ya Maragoli, iliyoitwa Maragoli Hills. Hata jamii yote ya Waluhya, kwa watu wa mbali kama Kuria wanaoishi na Wamaragoli waliohamia kule, husema Uluyani ni kwa Maragoli.

Sigadaki agandi ganyala kumeederera ku yaga. Vulavu vuenyekaanga kuliita “Maragoli”. Na vuladinyiiliza kali ilisavo liene Maragoli Cultural Festival, liikolekaanga vuli muhiga Disemba 26. Yee na ni giligali lisavo yili lijila lia kumanyya uvukulu – ilimanyikana liitu. Ulu ilimanyya liveeye uvukulu vua Mulogooli.

Hata hivyo juhudi za kutambua ujio wa jina “Maragoli” zinahitajika. Uchunguzi huo utatiliza mkazo jina Maragoli Cultural Festival, sherehe ambayo inaeziwa sana na Walogooli na hufanyika kila mwaka, Disemba 26. Ni ukweli sherehe hii ni ya “kuonyesha Ulogooli” kwa dunia asili na majivuno ya kijamii kama walivyofanya wanabiashara enzi za zama. Hivi sasa uonyeshaji ukiwa mafunzo na ustaarabu.

© Lung'afa Igunza, 2023/08/01

🕮 Getuma, Francis 2016. The Song of a Blacksmith and Totems of Abagusii. Nsemia Publishers.
🕮 Osogo, John 1966. A History of the Baluyia. London/New York/Nairobi: Oxford University Press.

Comments

Post a Comment